Connect with us

Soka

Dube nje wiki sita

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Azam fc Prince Dube anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa takribani wiki siku sita kutokana na kulazimika kufanyiwa operesheni ya maumivu anayoyasikia.

Dube amekuwa akisumbuliwa na maumivu chini ya tumbo tangu nusu fainali ya mchezo wa shirikisho dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora,baada ya kuumia alipelekwa Afrika Kusini kwa dokta Nicolas ambaye amekuwa akiwatibia wachezaji wa Azam fc,baada ya vipimo Dokta huyo alishauri achomwe sindano tu bila upasuaji.

Lakini mfumania nyavu huyo amekuwa akiendelea na maumivu kabla ya kuanguka na kushindwa kuendelea na mchezo wa kirafiki dhidi ya Kabwe Worriors ambao alifunga,na ndipo aliporudishwa tena bondeni ambapo safari hii dokta Nicolaus ameshauri afanyiwe upasuaji.

Dube atakosa michezo ya awali ya mtoano kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Horseed pamoja na michezo ya mwanzo ya ligi kuu soka Tanzania Bara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka