Connect with us

Makala

Diarra,Aucho Wakosekana Dhidi ya Namungo Fc

Kocha Sead Ramovic amelazimika kumuanzisha kipa Khomeini Abubakar kutokana na kukosekana kwa Kipa Djigui Diarra ambaye anasumbuliwa na maumivu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Klabu ya Namungo Fc.

Yanga sc ikiwa haijapata ushindi katika michezo miwili mfululizo ya ligi kuu ya Nbc nchini pia Inaendelea kuwakosa wachezaji wake Khalid Aucho na Ibrahim Bacca sambamba na Clement Mzize na Chadrack Boka kutokana na majeraha na adhabu ya kufungiwa kutokana na kuwa na kadi.

Pia kocha Ramovic amemuweka benchi mshambuliaji Prince Dube kutokana na sababu za kiufundi huku akiamua kumuanzisha Kennedy Musonda.

Beki Bakari Mwamnyeto ameanza kuchukua nafasi ya Bacca huku Duke Abuya akichukua nafasi ya Aucho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala