Connect with us

Soka

Chasambi Rasmi Simba Sc

Klabu ya Simba sc imemtambulisha rasmi kinda Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar kuwa mchezaji wa klabu hiyo baada ya kufanikiwa kununua mkataba wake uliosalia katika klabu ya Mtibwa sugar ambapo sasa atakua mchezaji wa klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Chasambi mchezaji bora wa ligi ya vijana wa miaka 20 kwa miaka miwili mfululizo amejiunga na Simba sc baada ya klabu hiyo kulipa kiasi cha Tsh.75 milioni zilizoko katika kipengele cha kununua mkataba wa mchezaji huyo katika klabu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar ambayo ilimpandisha kutoka timu za vijana za klabu hiyo.

Tayari baada ya kutambulishwa mchezaji huyo ameungana na kikosi cha klabu hiyo katika michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar ambapo ameanza mazoezi rasmi akisubiri kama atapangwa na kocha Abdelhack Benchika katika michezo inayofuata Visiwani humo.

Hii si mara ya kwanza kwa Simba sc kufanya biashara ya wachezaji na Mtibwa sugar ikikumbukwa kuwa iliwahi kuwasajili Salim Mbonde,Mzamiru Yassin,Mohamed Ibrahim na wengineo kuja kuhudumu klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka