Connect with us

Makala

C.E.O Namungo Akimbia Vipigo

Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Namungo Fc Omary Kaya ameamua kujiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na vipigo mfululizo ambavyo timu hiyo imevipata msimu huu.

Kaya ameandika barua ya kuachia ngazi baada ya timu yake kuruhusu kipigo cha mabao 2-0 kutoka Fountain Gate Fc siku ya Alhamis August 29 huku pia ikifungwa 2-1 na Tabora United katika uwanja wa nyumbani wa Majaliwa.

“Mimi Omary Kaya siku ya leo tarehe 30 August 2024 nimewasilisha kwa Uongozi barua ya kujiuzuru nafasi ya utendaji mkuu wa Klabu Namungo Fc”Ilisomeka taarifa hiyo huku ikiendelea kusema.

“Hivyo napenda kuwashukuru Uongozi,benchi la ufundi,wachezaji na mashabiki wote wa klabu ya Namungo katika kipindi chote nilichotumikia klabu kwa Ushirikiano wao kama familia”.

Kutokana na taarifa hiyo tayari klabu hiyo imekubali taarifa hiyo na kuthibitisha kukubaliana na barua hiyo ya kujiuzuru.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala