Connect with us

Makala

Beki Mkongo Rasmi Yanga sc

Klabu ya Yanga sc imemtambulisha rasmi Beki Chadrack Boka baada ya kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo akitokea klabu ya St.Eloi Lupopo Fc ya nchini Congo Dr ambapo anachukua nafasi ya Joyce Lomalisa aliyemaliza mkataba klabuni hapo.

Yanga sc imeamua kumsajili beki huyo baada ya kushindwana maslahi na Lomalisa Mutambala ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili akiisaidia kuchukua makombe ligi kuu na kombe la shirikisho mara mbili.

Boka atasaidiana na Nickson Kibabage katika eneo la beki wa kushoto katika michuano mbalimbali ambayo klabu ya Yanga sc itashiriki msimu ujao huku kocha Miguel Gamond akiwa na mtihani wa kuamua nani awe anaanza mara kwa mara kikosini humo.

Boka mwenye miaka 24 alijiunga na Fc Lupopo akitokea Sanga Balende Fc ya nchini humo humo ambapo pia aliicheza Tp Mazembe mwaka 2019 ambapo baada ya miaka mitatu ndani ya Fc Lupopo sasa amejiunga na Yanga sc.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala