Connect with us

Soka

Azam Fc Yajichimbia Nafasi ya Pili

Klabu ya Azam Fc imezidi kujihakikishia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuibamiza Jkt Tanzania kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Mei 21 katika uwanja wa Meja Jenerali Isamhyo ulioko Mbweni jijini Dar es salaam.

Azam Fc inakabiliwa na upinzani mkubwa wa kumaliza katika nafasi ya pili ya ligi kuu nchini kutoka Simba sc hivyo kupata alama tatu katika mchezo huo limekua jambo jema kwao huku ligi ikiwa imesaliwa na michezo miwili kutamatika.

Azam Fc ilipata bao la uongozi kutoka kwa Abdul Sopu dakika ya 30 akimalizia pasi nzuri ya Gibril Sillah ambapo aliunganisha krosi hiyo moja kwa moja na mpira kumshinda kipa wa Jkt Tanzania na kuzama nyavuni.

Jkt pamoja na kuwa wapo nyumbani hawakuonekana kuwapa upinzani wa kutosha Azam Fc ambapo asilimia kubwa walitawaliwa hasa eneo la kiungo huku dakika ya 90+5 Feisal Salum alipokea pasi safi ya Kipre Jr na kupiga shuti kali kuandikia Azam Fc bao la pili.

Azam Fc sasa wamefikisha alama 63 katika michezo 28 wakiwa katika nafasi ya pili huku Jkt Tanzania baada ya kipigo hicho sasa wamebaki nafasi ya 10 wakiwa na alama 31 katika michezo 28 ya ligi kuu ya Nbc nchini Tanzania

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka