Connect with us

Makala

Azam Fc Yaisambaratisha Coastal Union

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kocha Rachid Taoussi anazidi kudhihirisha umahiri wake baada ya kuendelea kumuamini mshambuliaji Nassoro Saiduni ambaye alifunga bao pekee katika mchezo huo akipokea pasi safi ya Feisal Salum na kuwachambua walinzi wa Coastal union na kufunga bao hilo dakika ya 9 ya mchezo huo.

Azam Fc baada ya dakika tisini za mchezo huo sasa imefikisha alama nane ikicheza jumla ya michezo minne ya ligi kuu ikiwa katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini huku Coastal Union ikiwa katika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na alama moja pekee huku ikicheza jumla ya michezo minne ya ligi kuu nchini.

Pamoja na ushindi huo bado Azam Fc inakibarua kizito cha kutafuta muunganiko wa timu pamoja na kikosi cha kwanza ambapo mpaka sasa kocha Taoussi hajapata uhakika wa kikosi kamili cha kwanza ambapo mara kadhaa amekua akiwaacha mastaa wengi wa kigeni kama mshambuliaji Jhonier Blanco.

Mchezo unaofuata kwa klabu hiyo utakua dhidi ya Klabu ya Simba Sc siku ya alhamis katika uwanja wa New Amaan complex Visiwani Zanzibar ambapo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala