Home Soka Yanga sc Yawasili Mbeya

Yanga sc Yawasili Mbeya

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuwasili salama jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa pili wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Kengold Fc utakaofanyika kesho Septemba 24 katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini humo.

Katika msafara huo uliokua na mastaa karibuni wote wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo uliwasili jioni ya Septemba 23 na kupokelewa na rundo la mashabiki wa klabu hiyo waliofika kwa magari ya kukodi na binafsi pamoja na pikipiki katika uwanja wa ndege wa Songwe jijini humo.

Msafara huo uliongozwa na viongozi wa klabu hiyo sambamba na kocha Miguel Gamondi ambaye alifurahishwa na kujitokeza kwa wingi kwa mashabiki hao.

banner

Yanga sc itacheza mchezo wake wa pili siku ya kesho kuwavaa Kengold baada kupata alama tatu kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar ikishinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Maxi Nzengeli na Clement Mzize.

Kengold Fc wenyewe wamecheza michezo minne na kupoteza yote na kuwafanya kuwa mkiani mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited