Connect with us

Soka

Azam FC yaanza vizuri kimataifa

Wwakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azam FC wameanza vema michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Horseed ya Somalia katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam complex Chamazi Dar es salaam na kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Horseed ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli dakia ya 22 kwa mkwaju wa adhabu likifungwa na Nor kabla ya Ayub Lyanga kuisawazishia Azam kwa kichwa dakika ya  32 na kwenda mapumziko wakiwa 1-1.

Azam walijipatia magoli mengine mawili kipindi cha pili dakika ya 73 kupitia kwa Idriss Mbombo na dakika ya 78 likigungwa na Lusajo Mwaikenda.

Ushindi huo ni muendelezo wa matokea mazuri kwa timu za Tanzania Bara katika hatua za awali zza mtoano za kimbe la shirikisho baada ya hapo japo wawakilishi wengine Biashara United kupata matokeo ugenini ya 1-0 .

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka