Connect with us

Soka

AGUERO; Barca noma wabania hadi umeme

Mchezaji mpya wa Fc Barcelona Sergio Aguero amesema kushangazwa na utaratibu wa timu yake hiyo mpya ya ubanaji wa matumizi kwani ni hali ambayo hakuwahi kukutana nayo alipokuwa Man city.

Aguero amesema kuwa alipokuwa Man city walikuwa wakiruhusiwa kufika viwanja vya mazoezi hata saa moja na nusu kabla ratiba ya mazoezi kuanza,tofauti na Barcelona ambapo wanatakiwa kufika viwanja vya mazoezi nusu saa kabla ya mazoezi ya siku kuanza rasmi.

Aguero aliendelea kuwa alipofika viwanja vya mazoezi mapema alfajiri saa moja kabla ya mazoezi aliwasha taa lakini mchezaji mwenza ambaye ni nahodha msaidizi wa Barcelona Gerard Pique alimwambia azime kwani yeye hataki tena kukatwa mshahara wake.

Hali hiyo inaonesha kuwa Barcelona wanajaribu kupunguza matumizi kutokana na hali ngumu inayopitia klabu hiyo kutokana na kuandamwa na madeni makubwa hali iliyosababisha hadi kumpoteza mchezaji wao nyota Lionel Messi aliyetimkia PSG.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka