Connect with us

Soka

28 Yanga sc Kimataifa

Klabu ya Yanga sc imewasilisha orodha ya wachezaji 28 itakaowatumia katika michuano ya kimataifa hasa katika hatu ya awali ya mtoano itakapomenyana na Rivers United ambayo watakutana jumapili Septemba 12.

Licha ya vilabu vinavyoshiriki michuano hiyo kuruhusiwa kusajili wachezaji 40 lakini klabu hiyo imepeleka majina 28 pekee huku ikiwaacha nyota kama Balama Mapinduzi na Yassin Mustapha.

Orodha ambayo Yanga imewasilisha inawajumuisha makipa 3 ambao ni Diarra Djigui, Erick Johola na Ramadhan Kabwili huku mabeki wakiwa 9 ambao ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yannick Bangala, Dickson Job, Bakari Mwammnyeto.

Wengine ni Kibwana Shomari, Djuma Shaban, David Bryson, Adeyun Saleh na Paul Godfrey ‘Boxer’ watakaosimamia uimara wa Yanga katika safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Yanga imewajumuisha viungo 6 ambao Mukoko Tonombe, Aucho, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Deus Kaseke, Jesus Muloko, Farid Mussa, huku kwenye eneo la ushambuliaji itakuwa na watu 5 ambao ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Yacouba Songne, Said Ntibazonkiza na Yusuf Athuman.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka