Connect with us

Other Sports

Ulimwengu Matatani Drc

Mshambuliaji wa timu ya Tp Mazembe  Thomas Ulimwengu ameshukiwa na kocha wa timu hiyo Mihayo Kazembe kutokana na kushuka kiwango katika michezo kadhaa ya timu hiyo tofauti na msimu uliopita ambapo alikua moto wa kuotea mbali.

Kazembe anasema licha ya kumpa nafasi mara nyingi mshambuliaji huyo lakini anakosa umakini kwa kiasi kikubwa hivyo anafikiri kutafuta mbadala wake kwa ajili ya kuongeza makali kikosini humo.

Ulimwengu licha ya kucheza katika klabu hiyo katika michuano ya kimataifa amekosa nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kutokana na kocha Kim Poulsen kutoridhishwa na kiwango chake.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Other Sports