Connect with us

Makala

Kabwili Aiponza Rayon Sports

Shirikisho la soka Duniani (Fifa) limeifungia klabu ya Rayon Sports ya Rwanda kufanya usajili wa wachezaji wa kigeni baada ya kukutwa na hatia ya kutomlipa stahiki zake aliyekuwa golikipa wao Ramadhan Kabwili.

Golikipa huyo wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars, alijiunga na Rayon Sports kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini baadae aliamua kuondoka kabla ya mkataba kumalizika kutokana na kutolipwa mshahara wake kwa kipindi cha miezi minne.

Barua hiyo iliyotumwa kwa shirikisho la soka nchini Rwanda huku nakala ikitumwa kwa klabu hiyo pamoja na mlalamikaji Ramadhani Kabwili pia limeiagiza shirikisho la soka nchini humo kuifungia klabu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wa ndani kwa mujibu wa sheria na taratibu za shirikisho hilo kwa wanachama wake.

Kwa sasa Kabwili yupo nchini Tanzania akiwa bado hana timu yoyote lakini yupo tayari kurudi uwanjani ikiwa kuna timu inahitaji huduma yake na kufikia makubaliano ya usajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala