Connect with us

Makala

Yondani Anukia Kagera Sugar

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc Kelvin Yondani yupo njiani kujiunga na klabu ya Kagera Sugar akitokea klabu ya Geita Gold Fc ambapo amedumu kwa takribani nusu msimu pekee alipojiunga akitokea Polisi Tanzania.

Yondani yupo kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba wake na Geita Gold Fc ili akamilishe usajili huo wa kujiunga na Kagera Sugar ambayo imekua na matatizo kadhaa katika safu ya ulinzi ambayo imekua ikilegalega mara kadhaa.

Yondani ni beki mzoefu nchini ambapo alifanikiwa kuichezea klabu ya Yanga sc na timu ya Taifa kwa muda mrefu akiwa kama nahodha pia hivyo uzoefu huo utaenda kuisaidia Kagera Sugar Fc kuimarisha eneo la ulinzi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala