Connect with us

Makala

Wawa Aondoka Singida Big Stars

Beki wa zamani wa klabu ya Simba sc Serge Paschal Wawa ameondoka katika klabu ya Singida Big Stars baada ya kumalizana na klabu hiyo aliyojiunga nayo akitokea klabu ya Simba sc ambapo amedumu kwa takribani nusu msimu  pekee.

Wawa kwa mara ya kwanza alitambulishwa na Azam Fc nchini misimu kadhaa nyuma miaka ya 2014 ambapo alidumu Azam Fc kwa misimu miwili kabla ya kujiunga tena na El-Merrekh Fc ya nchini Sudan alipotokea kisha akajiunga na Simba sc alipokaa kwa miaka mitano mpaka msimu huu mwanzoni alipojiunga na Singida Big Stars.

Wawa ameondoka klabuni hapo baada ya kushindwa kuwa na kiwango bora ambapo mara kadhaa amesababisha timu hiyo kufungwa kutokana na kukosa umakini katika kutuliza mashambulizi ya wapinzani ambapo klabu hiyo imemsajili beki mpya kutoka Brazil Marcos Wilson da Silva kuziba nafasi hiyo ambaye atashirikiana na Biemesi Carno.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala