Connect with us

Makala

Yanga SC vs Rivers Utd bila mashabiki

Mabingwa wa kihistoria Tanzania klabu ya Yanga imetoa taarifa rasmi kupitia kurasa zake za kijamii kuwa mchezo wa awali hatua ya mtoani wa klabu bingwa Afrika dhid ya Rivers United ya Nigeria utachezwa bila ya uwepo wa mashabiki uwanjani.

Mchezo huo utafanyika Jumapili hii ya Septemba 12 katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam kuanzia saa kumi na moja jioni.

Awali klabu ya Yanga ilitoa orodha ya viingilia vya mchezo huo kabla ya kupokea taarifa rasmi kutoka CAF kupitia shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) kuwa mechi za awali za mtoano zitapigwa bila mashabiki uwanjani.

Hilo ni pigo kubwa kwa Yanga kuelekea kurejea kwenye michuano ya kimataifa kwani iliwahitaji sana mashabiki wake kipindi hiki katika kuchagiza na kuwapa hamasa wachezaji wake kupambana na kupata matokeo katika uwanja wa nyumbani.

Katika hatua nyingine TFF nao wametoa taarifa ya kuvitaka vilabu vyake vinavyoshiriki michuano ya kimataifa kuheshimu maamuzi hayo na kuwa wao kama chama cha soka watapambana kuhakikisha kuwa mashabiki wanaruhusiwa katika michezo ijayo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala