Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho la Crdb baada ya kuifunga Tabora United 3-0 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam.
Yanga sc ikianza na safu ya ushambuliaji ya Clement Mzize na Aziz Ki ilipata shida kulifikia lango la Tabora kutokana na timu hiyo kucheza nyuma zaidi huku umahiri wa kipa John Noble ukiwa kikwazo kwa Yanga sc kupata bao.
Azizi Ki akicheza mbele ya mama yake alifanikiwa kuipatia Yanga sc bao la kwanza dakika ya 35 ya mchezo kwa shuti kali ambapo mpaka mapumziko matokeo yalibaki hivyo hivyo.
Dakika ya 65 Kennedy Musonda alifunga bao la pili akimalizia kazi nzuri ya Guede alipiga shuti lilipanguliwa na Kipa John Noble na kumkuta mfungaji huku Guede akifunga bao la tatu kwa pasi nzuri ya Pacome Zouzou baada ya beki kushindwa kuokoa mpira kwa usahihi.
Yanga sc baada ya ushindi huo sasa watakutana na Ihefu Fc ambao waliwafunga Mashujaa Fc 4-3 katika changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa nusu fainali.
Pia katika mchezo mwingine wa robo fainali ya michuano ambapo Coastal union iliibuka vinara mbele ya Geita Gold baada ya kushinda bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.