Connect with us

Makala

Sowah Kupishana na Guede Singida Bss

Mshambuliaji Jonathan Sowah yupo mbioni kujiunga na timu ya Singida Black Stars akichukua nafasi ya Joseph Guede ambaye amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na klabu hiyo.

Sowah ambaye anaichezea Al Ahli Benghaz ya nchini Libya anajiunga na klabu hiyo baada ya timu hizo mbili kufikia makubaliano ya dau la dola 200,000 za kimarekani ambapo ilisemekana kuwa staa huyo atajiunga na Black Stars wakati wa dirisha hili la usajili.

Taarifa kutoka ndani ya Singida Black Stars zinasema kuwa Sowah anakuja kuungana na Elvis Rupia kama washambuliaji kinara wa klabu hiyo ambapo anatarajiwa kupokea mshahara kiasi cha dola elfu tano ambapo atakua moja ya mastaa wanaopokea mshahara mkubwa klabuni hapo.

Mpaka sasa Singida Black Stars ina alama 30 katika ligi kuu ya Nbc nchini ikiwa imecheza jumla ya michezo 14 ya ligi kuu katika nafasi ya pili nyuma ya Azam Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala