Connect with us

Makala

Simba Yashinda 3-0

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa ligi kuu nchini uliomalizika jioni ya leo katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Simba sc iliwaanzisha John Bocco,Pape Osmane Sakho,Pater Banda na Cletous Chama katika eneo la ushambuliaji huku eneo la kiungo wa chini wakicheza Mzamiru Yassin na Erasto Nyoni safu ambayo ilicheza kikubwa na kufanikiwa kupata mabao matatu katika mashuti matatu ya kwanza kulenga lango.

Pape Osmane Sakho alikua wa kwanza kuandika bao dakika ya 9 huku Mzamiru Yassin akiongeza la pili dakika ya 14 na Cletous Chama akafunga bao la tatu dakika ya 18 na kumaliza mechi mapema kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili ikishuhudiwa Meddie Kagere akikosa penati.

Simba sc sasa inafikisha alama 34 tofauti ya alama 8 dhidi ya Yanga sc waliopo kileleni huku Biashara united wakizidi kujichimbia shimo wakiwa mkiani mwa msimamo wa ligi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala