Connect with us

Makala

Simba sc Yawasili Ruangwa

Klabu ya Simba sc imewasili salama mkoani Mtwara katika wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaofanyika katika uwanja wa Majaliwa uliopo wilayani humo siku ya kesho Jumatano jioni.

Simba sc iliwasili kwa basi wilayani humo ikiwa na kumbukumbu ya kutolewa katika michuano ya kimataifa kwa penati na Wydad Casablanca wikiendi iliyopita na sasa imeelekeza nguvu zake kuhakikisha inalinda heshima kwa kutwaa taji la ligi kuu linalomilikiwa na Yanga sc.

Simba sc na Namungo ni klabu zilizo na uwezo wa kupambana huku kila klabu inaweza kupata matokeo ya ushindi dhidi ya mwenzake kutokana na kuwa na wachezaji bora na imara kwa kila upande huku nguvu ya pesa ikiwepo.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu nchini Simba sc ipo katika nafasi ya pili ikiwa na alama 63 huku Namungo ikiwa nafasi ya sita na alama 35 huku timu zote zikiwa zimecheza jumla ya michezo 26.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala