Connect with us

Makala

Simba Sc Yatoka Kiume Caf

Pamoja na kwamba imetolewa katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika wadau wamichezo nchini wameipongeza klabu ya Simba sc kwa kuonyesha kiwango kikubwa katika mchezo wa hatua ya robo fainali nchini Afrika ya kusini dhidi ya Orlando Pirates ya nchini humo kiasi cha kutolewa kwa njia ya matuta 4-3.

Katika mchezo huo wa marudiano Simba sc ilihitaji ushindi ama sare ili kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuwa na mtaji wa bao 1 kutokana na ushindi wa hapa nyumbani.

Kocha Pablo Franco aliamua kuingia na mabeki sita kwa wakati mmoja akiwajumuisha Shomari Kapombe,Mohamed Hussein,Serge Wawa,Henock Inonga na Joash Onyango pamoja na Israel Mwenda ambapo walifanikiwa kuzuia kwa dakika 60 ambapo Kwame Peprah alifunga kwa kichwa na kusababisha mchezo kumalizika kwa matokeo ya jumla ya 1-1 na kuingia hatua ya matuta.

Jonas Mkude na Henock Inonga walikosa matuta huku Shomari Kapombe,Meddie Kagere na Mohamed Hussein wakipata na kwa upande wa Orlando Pirates Mnamibia Deon Hotto, Mmalawi Frank Mhango, Tshegofatso Mabasa and Ofori walifunga penati zao.

Timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali ya kombe hilo ni Orlando Pirates,Tp Mazembe,Al Ahly Tripoli na Rs Berkane ambapo zinatarajiwa kuwania kuingia fainali ya kombe hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala