Connect with us

Makala

Simba Sc Yaisubiri Namungo Fc

Klabu ya Simba sc kesho inatarajiwa kumalizia hasira kwa Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini utakaofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam majira ya saa kumi jioni baada ya kufungwa 5-1 na Yanga sc.

Simba sc mpaka sasa hali haijatulia kutokana na kipigo hicho kutoka kwa watani wao wa jado hivyo kulazimika kushinda mchezo wa kesho ili kurejesha furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Katika mchezo huo Simba sc itaingia ikiwa chini ya benchi jipya la ufundi chini ya mwalimu Dani Cadena pamoja na Selemani Matola baada ya kocha Roberto Oliveira maarufu kama Robertinho kutimuliwa kutokana na kipigo kizito kutoka kwa Yanga sc.

“Tumewaandaa wachezaji vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Namungo Fc huku tukiwa tunawaheshimu na kuwafatilia wapinzani wetu hivyo tunategemea mchezo mgumu lakini tumejipanga kupata ushindi”Alisema Cadena akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo

Nae nahodha wa Simba sc John Bocco alisema kuwa wao kama wachezaji wapo tayari kwa mechi hiyo “Wachezaji wote maandalizi yetu ni mazuri kuelekea kwenye huu mchezo kuhakikisha tunapata alama tatu na tumejiandaa kulingana na mpinzani ambaye tunakutana nae ili kupata ushindi”.

Kwa upande wa Namungo Fc iliyochini ya kocha Dennis Kitambi ambaye alichukua timu baada ya mwalimu Cedrick Kaze kutimuliwa yeye alisema kuwa watawashambulia nzima ili kupata bao kwa wanafungika.

“Al Ahly , Yanga SC wametupa njia ya kupita, Simba SC michezo mitatu ya nyuma wameruhusu mabao nane (8) 2-2, 1-1, 5-1 na sisi tunaanzia hapo, faida tuliyokuwa nayo sisi Namungo Fc ni Simba Sc inaruhusu mabao hivyo tunaweza kupata bao na tunaichukua fursa hii kuwashambulia” amesema kocha Denis Kitambi.

“Kuna muda mwingine hauhitaji kuwa mbunifu sana sisi tutapita njia ambazo wamefanya Al Ahly na Yanga SC, Al Ahly na Yanga SC wametupa mfano wa namna ya kudili na Simba SC”- ameendelea kusema kocha huyo.

Simba sc itakua na kibarua kigumu katika mchezo wa kesho kutokana na kusumbuliwa na presha za mashabiki wa klabu hiyo hasa baada ya kipigo cha jumapili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala