Klabu ya Simba Sc imemtangaza Bi Zubeda Hassan Sakuru kuwa Kaimu mtendaji mkuu wa Klabu hiyo akichukua nafasi ya Francois Regis ambaye imesitisha mkataba wake kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi na klabu hiyo.
Awali Simba sc ilimtangaza Regis aliyekua mtendaji mkuu wa zamani wa klabu ya Apr Fc ya Rwanda kuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Iman Kajula ambaye mkataba wake ulikua ukifikia tamati.
Hata hivyo tangu atangazwe kuchukua nafasi hiyo pindi mkataba wa Kajula utakapofika mwisho mwezi Augusti mwaka huu Regis alikua hajaanza majukumu yake kutokana na sababu mbalimbali ambapo inasemekana ikiwemo changamoto ya vibali vya kufanyia kazi nchini.
Zubeda anakaimu nafasi hiyo mpaka pale klabu hiyo itakapokamilisha Mchakato wa kumpata mtendaji mkuu mpya huku pia uzoefu wa kufanya kazi kama msaidizi wa Kajula katika upande wa miradi ukimbeba mwanadada huyo ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu akiwa katika mwaka wa mwisho kukamilisha masomo hayo.
Mwanadada huyo pia ni mhitimu wa shahada ya awali ya Utawala wa Umma kutoka chuo kikuu cha Mzumbe nchini Tanzania.
Zubeda anakua mwanamke wa pili katika historia ya klabu hiyo kushika nafasi hiyo akitanguliwa na Babrah Fernández aliyedumu kabuni