Connect with us

Makala

Simba sc Waikalisha Namungo Fc

Licha ya mashabiki wa klabu ya Simba sc kukosa imani na kikosi chao bado kikosi hicho kimeweza kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo Fc mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc ikianza na kikosi kamili cha Aishi Manula,Shomari Kapombe na Mohamed Hussein huku mabeki wa kati wakiwa ni Joash Onyango na Henock Inonga na kiungo kikiongozwa na Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin huku eneo la ushambuliaji likiwa na Moses Phiri,Augustine Okrah,Kibu Dennis na Pape Sakho ambapo dakika ya 31 ya mchezo ilifanikiwa kupata bao baada ya Mohamed Hussein kuwazidi ujanja mabeki wa Namungo na kumpasia Phiri aliyefunga kiulaini kabisa.

Licha ya bao hilo Simba sc ilijenga mashambulizi mengi langoni mwa Namungo Fc walionekana kuzidiwa kasi na maarifa hasa eneo la katikati mwa uwanja lakini kukosa utulivu kwa Kibu Dennis na Pape Sakho kuliwanyima Simba sc mabao kadhaa.

Kutokana na ushindi huo sasa Simba sc imepanda mpaka nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama 24 katika michezo 11 ya ligi kuu huku Azam Fc ikiwa nafasi ya kwanza ikiwa na alama 26 katika michezo 12 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala