Connect with us

Makala

Salamba Atua Misri

Mshambuliaji wa klabu ya Namungo Fc Adam Salamba amesajili na klabu ya Ghazl-El Mahala inayoshiriki ligi kuu nchini Misri kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo ataungana na Mtanzania Himid Mao kuhudumu katika klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Misri ikiwa imeanzishwa mwaka 1936.

Klabu hiyo ni moja ya klabu kongwe nchini humo ikiwa inapatikana maeneo ya El Mahalla El Kubra na imemaliza ligi kuu msimu uliopita katika nafasi ya 15 ikiwa na alama 36 katika michezo 34 ya ligi kuu nchini humo.

Salamba mchezaji wa zamani wa klabu ya Namungo Fc,Simba sc na Js Soura ya nchini Algeria anajiunga na klabu hiyo akiwa kama mchezaji huru baada ya kukaa bila timu kwa miezi ya hivi karibuni na tayari klabu hiyo imeshamtambulisha kwa mashabiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala