Connect with us

Makala

Saido Afanya Maajabu Simba sc

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Saido Ntibanzokiza ameendelea kufanya maajabu tangu ajiune na klabu ya Simba sc akitokea klabu ya Geita Gold Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu baada ya kuwa na takwimu nzuri na za kuvutia licha ya kuwa na umri mkubwa.

Saido ambaye ametoka kuisaidia Simba sc kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya city akifunga mabao mawili kati ya matatu huku moja likifungwa na Pape Osmane Sakho alifikisha jumla ya mabao tisa ya ligi kuu baada ya kufunga huku pia akiwa na assista nane katika ligi kuu msimu huu.

Mchezaji huyo alijiunga na Simba sc akiwa tayari amefunga mabao manne  na assisti tano za mabao lakini tayari amesaidi upatikanaji wa mabao mawili na kufunga matano katika michezo miwili alicheza akiwa na Simba sc ambapo katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alifunga mabao matano na kuassist upatikanaji wa bao la kwanza kwa John Bocco.

Simba sc baada ya kuifunga Mbeya city sasa imefikisha alama 47 katika michezo ishirini la ligi kuu ya Nbc huku itakua na kibarua kigumu dhidi ya Dodoma jiji Fc ugenini katika mchezo ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala