Connect with us

Makala

Ronaldo Apiga nne mbele ya Messi

Cristiano Ronaldo alivaana na Lionel Messi,Neymar na Mbappe katika mchezo wa kirafiki baina ya Psg dhidi ya kombaini ya timu za Al Hilal na Al Nassr uliofanyika katika umoja wa nchi za kiarabu ambapo Psg iliibuka na ushindi wa magoli 5-4 huku Ronaldo na Messi wakifunga mabao.

Licha kufungwa kwa mabao 5-4 Ronaldo ameondoka na faraja akifunga mabao mawili peke yake dakika za 34 na 45 za kipindi cha kwanza huku Lionel Messi akifunga dakika ya 2 ya mchezo huku mabao mengine ya Psg yakifunwa na Marquinhos 43′,Sergio Ramos 54′ na Kylian Mbappe dakika ya 60 na la mwisho likifungwa na Hugo Ekitike dakika ya 78.

Hyun-Soo Jang aliipatia bao kombaini ya Al Riyadh dakika ya 56 huku pia Talisca nae akifunga dakika ya 90 na kuufanya mchezo huo kuwa wa 11 kwa Ronaldo kushinda dhidi ya Lionel Messi katika mechi 36 walizokutana kama wachezaji wa timu tofauti tofauti.

Licha ya kuachwa na Manchester United mwezi Novemba na kutocheza mechi yeyote tangu ajiunge na Al-Nasrr Ronaldo alifanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo ya kirafiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala