Connect with us

Makala

Ronaldo kinara kwa mkwanja duniani

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano ametajwa na jarida la tafiti ya masuala ya kiuchumi la Forbes kuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi duniani kwasasa akiingiza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 125 kwa mwaka.

Ronaldo anapata dola milioni 70 kupitia kama mshahara na bonasi kwenye timu anayochezea wake na kiasi cha dola milioni 55 kupitia mikataba ya kibiashara aliyoingia na makampuni binafsi.

Mshindani wake wa muda mrefu Lionel Messi anashika nafasi ya pili akiingiza dola milioni 11o kupitia mshahara na mikataba ya kibiashara huku Mbrazil Neymar akifunga tatu bora ya wanasoka wenye waliopata mkwanja mrefu 2021 akijichotea dola milioni 95.

Mohamed Salah anaongoza kwa wanasoka kutoka Afrika akiingiza dola milioni 41 kwa mwaka huku akishika nafasi ya 5 duniani.

Ifuatayo ni orodha ya wanandinga 10 duniani walioingiza mkwanja mrefu kwa mwaka 2021.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala