Connect with us

Makala

Rais Samia Akutana na Bosi wa Man Utd

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na bosi wa Timu ya mpira wa Miguu ya Manchester United Sir Jim Ratcliffe ya Uingereza leo ikulu jijini Dar es Salaam.

Mbali na mkutano huo pia Rais Samia alikabidhiwa jezi ya klabu hiyo iliyosainiwa na Wachezaji wa Timu hiyo kutoka kwa Mmiliki wa Klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili, 2025.

Katika mazungumzo hayo mmiliki wa klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe ameeleza dhamira yake ya kuitumia Klabu yake kutangaza utalii nchini Tanzania. Rais Dkt. Samia pia amemkaribisha Mmiliki huyo wa Club ya Manchester kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini.

Ratcliffe ni mwanzilishi wa kampuni ya Six Rivers ambayo inajihusisha na uhifadhi pamoja na mambo ya utalii ambapo amekutana na Rais Samia pamoja na mashabiki wa klabu ya Manchester United jijini Dar es Salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala