Connect with us

Makala

Pochettino Yu Huru Sasa

Kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino sasa yuko huru kujiunga na klabu yoyote anayoitaka bila vikwazo kutoka kwa waajiri wake baada ya marufuku ya miezi sita yaliyomzuia kufanya hivyo kukamilika.

Tottenham ilizuia klabu yoyote kumnyakua kocha huyo kabla ya miezi sita kukamilika kwa kuweka sharti kuwa klabu inayomtaka lazima ilipe timu hiyo kutoka kaskazini mwa London milioni 34.6 ndipo imuajiri mwamba huyo kwa sababu ilikuwa imemlipa Pochettino fidia ya kumtema kabla ya kandarasi kumalizika.

Kukamilika kwa miezi hiyo kunamweka Pochettino huru kuchukuliwa na klabu yoyote bila ya ada kutolewa kwa mabosi wa Tottenham Hotspurs.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala