Connect with us

Makala

Wanao Maliza Mikataba,Wasubiri Ligi Imalizike

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Wanachama kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rahim Shabany amesema kwa wale wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni na kumalizika mwezi huu watabaki kuwa mali ya timu hadi ligi itakapo malizika.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba, kisheria kama ligi inaendelea lazima wamalizie msimu na baada ya hapo watakuwa huru kama mchezaji kuna timu anahitaji kwenda atafanya hivyo mwishoni.

“Tuchukulie kuna mchezaji anayechezea Mtibwa halafu kutokana na hali hii akasajiliwa  Lipuli na tunakwenda kumalizia mechi za msimu huu hapo utaona kuna mkanganyiko, hivyo lazima amalize msimu na timu yake”alisema Shabany.

Hivi karibuni Fifa ilitolea Ufafanuzi kuhusu jambo hilo la mikataba ya wachezaji wanaomaliza mikataba yao kusubiri hadi pale ligi za nchi zao zitakapomalizika baada ya kuahirishwa kutokana na janga la corona linaloitikisa dunia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala