Connect with us

Makala

Ni Simba Sc vs Singida Black Stars

Klabu za Simba sc na Singida Black Stars zijatarajiwa kumenyana vikali katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb nchini katikati ya mwezi ujao.

Mchezo huo utazikutanisha timu hizo baada ya kila moja kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali baada ya timu hizo kupata ushindi na kufuzu moja kwa moja.

Simba sc siku ya Jumamosi April 11 2025 ilifanikiwa kuwafunga Mbeya City Fc kwa mabao 3-1 kupitia kwa Fabrice Ngoma, Lionel Ateba na Joshua Mutale ambapo Mbeya City walitangulia kupata bao kwa shuti kali la Mudathir Said.

Jumatatu April 14 Singida Black Stars nao walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Timu ya Kagera Sugar kwa mabao ya Victorien  Adebayor pamoja na Jonathan Sowah.

Kutokana na ushindi huo,Ratiba ya michuano hiyo inaonyesha kuwa timu hizo zitakutana kati ya Mei 15,16 au 17 kwa ajili ya mchezo huo wa nusu fainali unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Ugumu wa mchezo huo unatokana na kila kikosi cha timu hizo kusheheni mastaa wa maana wa ndani na wale wa kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala