Connect with us

Makala

Nabi Hakijaeleweka Yanga sc

Inasemekana kocha wa klabu ya Yanga sc Nasredine Mohamed Nabi badao hajasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo baada ya mazungumzo baina ya pande mbili kutofikia muafaka wa kusaini mkataba mpya.

Licha ya mazungumzo hayo tayari kocha huyo ana ofa mkononi kutoka klabu ya Far Rabat ya nchini Morroco ambayo imemuwekea mshahara wa takribani milioni 90 kwa mwezi.

Taarifa za ndani zinasema kuwa kocha huyo ana mpango wa kuendelea kusalia Yanga sc ili kutengeneza Cv ya kutosha lakini kama klabu hiyo itatimiza baadhi ya matakwa yake anayoyataka katika mkataba wake wa sasa baada ya kufanikisha kuwapatia mataji matatu makubwa nchini kwa msimu uliopita.

Nabi alijiunga na Yanga sc msimu wa 2021 baada ya klabu hiyo kuachana na kocha Cedric Kaze ambapo alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu ambao umeisha msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala