Connect with us

Makala

Simba sc Yalamba Dili Nono

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kupata udhamini mnono wa kutoka kampuni ya kubashiri ya M-beti ambayo ndiyo itakua mdhamini mkuu wa klabu hiyo yenye jina kubwa Afrika kwa sasa.

Simba sc imepata udhamini wa miaka mitano kutoka kwa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba na kampuni ya Sportspesa ambayo ilidhamini klabu hiyo pamoja na watani wao wa jadi Yanga sc kwa muda wa miaka mitano iliyopita kwa gharama ya shilingi bilioni 5 kwa kila mmoja.

Yanga sc yenyewe iliamua kuendelea na udhamini wa kampuni ya Sportspesa ambayo imeweka kiasi cha shilingi bilioni 12 kwa mkataba wa miaka mitatu huku Simba sc ambayo imeamua kuingia makubaliano na wapinzani wa kampuni hiyo ambayo ni M-bet wenyewe watalamba kiasi cha bilioni 26 katika mkataba wa miaka mitano.

Kampuni hiyo inaingia kama mdhamini mkuu wa klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake na Sportpesa na mgawanyo wa fedha utakuwa kama ifuatavyo;

Mwaka wa kwanza – Sh4.670 bilioni
Mwaka wa pili – Sh4.925 bilioni
Mwaka wa tatu – Sh5.205 bilioni
Mwaka wa nne – Sh5.514 bilion
Mwaka wa tano – Sh5.853 bilioni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala