Connect with us

Makala

Mtibwa Waboresha Benchi La Ufundi

Uongozi wa Mtibwa Sugar umefanya maboresho katika benchi lake la ufundi leo Agosti 28,kwa ajili ya msimu wa 2020/2021 unaotarajiwa kuanza Septemba 6.

Mabosi hao wamemteua Zubery Rashid Katwila kuendelea kukiongozi kikosi cha Mtibwa Sugar kama kocha mkuu akisaidiana na Vicent Barnabas ambaye awali alikuwa kocha mkuu wa timu ya Vijana.

Mtibwa Sugar imefanya pia mabadiliko katika nafasi ya kocha wa makipa kwa kumtambulisha Soudy Slim aliyewahi kuwa mchezaji wa Mtibwa sugar huku daktari wa timu akiwa ni Lawrance Mushi.

Wengine ni Amir Abdallah ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi wa vifaa vya timu na meneja wa timu ni David Chitty B’-goya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala