Connect with us

Makala

Morrison Kutua Kengold Fc

Nyota wa zamani wa klabu za Simba Sc na Yanga Sc Bernard Morrison yupo mbioni kujiunga na Klabu ya Kengold Fc yenye makazi yake Wilayani Chunya Jijini Mbeya.

Nyota huyo raia wa Ghana anajiunga na miamba hiyo ya Mbeya kwa mkataba wa miezi 6 kama mchezaji huru ukiwa ni moja ya mikakati ya mabosi wa klabu hiyo kuiepusha kushuka daraja.

Lengo la kumsajili staa huyo ni kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo inayoshika mkia katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Kocha mkuu wa Kengold Fc Omary Kapilima ameonekana kuvutiwa na staa huyo huku akijipanga kumdhibiti upande wa nidhamu ambapo mchezaji huyo amekua na matukio mengi nje ya uwanja ambayo huathiri kiwango chake mara nyingi.

Mbali na Morrison mabosi hao wanaangalia uwezekano wa kusajili mastaa wengine wenye uzoefu akiwemo Obrey Chirwa na Kelvin Yondani.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini klabu hiyo mpaka sasa ipo katika nafasi ya mwisho ikiwa na alama sita pekee katika michezo 16 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala