Connect with us

Makala

Mkude,Metacha Mazoezini Yanga sc

Staa Jonas Mkude na Metacha Mnata wamejiunga na wenzao katika viwanja vya mazoezi vya Avic Town pamoja na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu nchini ambapo Oktoba 25 wanatarajiwa kuwavaa Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu.

Mkude ameonekana katika mazoezi hayo katika kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo huku Metacha akionekana katika mazoezi ya kambi ya timu ya Taifa ya Tanznia (Taifa Stars) hasa baada ya kutoonekana katika misafara miwili ya timu kuekea Mbarali kuivaa Ihefu Fc na ule wa kuelekea jijini Mwanza kuwavaa Geita Gold Fc.

Taarifa za awali klabuni hapo zilisema kuwa mastaa hao walikua na matatizo ya kifamilia lakini pia taarifa zisizorasmi zinasema kuwa wachezaji hao walikua wamesimamishwa na kocha Miguel Gamondi kutokana na utovu wa nidhamu hasa baada ya kuchelewa kuripoti mazoezini.

Mkude na Metacha ni wachezaji waliojiunga na klabu hiyo msimu huu ambapo Mkude alitemwa Simba sc huku Metacha akisajiliwa kutoka Singida Big Stars.

Mpaka sasa bado haijafahamika rasmi upi ni ukweli kutokana na mijadala mbalimbali inayoendelea katika mitandao ya kijamii baada ya wawili hao kuonekana katika kambi ya mazoezi ya klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala