Connect with us

Makala

Mbuna Akimbilia Tanzania Prisons

Mchezaji wa zamani wa Yanga Sc na Majimaji FC Fred Mbuna, amejiunga na Tanzania Prisons kama kocha msaidizi wa timu hiyo ambayo Disemba 28, 2024 ilitangaza kuvunja mkataba wa aliyekuwa kocha wao mkuu Mbwana Makata.

Mbuna kabla ya kujiunga na Tanzania Prisons alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Yanga Princess akisaidiana na kocha Edna Lema.

Kocha huyo anaenda kuungana kocha Amon Jossiah ambaye amechukua nafasi hiyo kikosini akichukua nafasi ya Mbwana Makata ambaye alitimuliwa kutokana na matokeo mabaya.

Katika msimamo wa ligi kuu nchini mpaka sasa Tanzania Prisons imecheza michezo 16 ikiwa na alama 14 katika nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala