Connect with us

Makala

Mangalo Atua Singida Big Stars

Beki wa Biashara United ya mkoani Mara ambayo imeshuka daraja AbdulMajid Mangalo amekamilisha usajili kujiunga na klabu ya Singida Big Stars kwa mkataba wa miaka miwili huku akiziacha ofa za kujiunga na timu kubwa katika jiji la Dar es salaam.

Mangalo anayesifika kwa kutumia maarifa na akili pamoja na matumizi ya nguvu pale inapobidi amekua muhimili kwa muda mrefu katika kikosi cha Biashara United japo klabu hiyo imeshuka daraja kutokana na kutofanya vizuri katika ligi kuu msimu ulioisha.

Beki huyo pia amefunguka jinsi ilivyokua ngumu kukataa ofa za timu hizo lakini ilimlazimu kuzikacha kutokana na ushauri kutoka kwa wanafamilia na marafiki ambao mara nyingi humsaidia katika kufanya uamuzi wa baadhi ya mambo.

“Kwa hiyo siwezi kufanya maamuzi ya moja kwa moja bila ushauri wa ndugu zangu wananishauri na mwenyewe huchanganua hivyo niliona ni sahihi,” alisema na kuongeza;.

“Kwa sababu zile timu ukiangalia bado zina presha kubwa, zinataka kutengeneza timu na zinataka matokeo lazima presha iwe kubwa, hivyo ofa ya Simba ilipokuja nilishirikisha familia yangu ambayo ilinishauri nicheze kwanza huku chini hata miaka miwili nitakuwa nimekomaa na presha ya timu hizo,” alisema.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala