Connect with us

Makala

Bangala Atua Dodoma Jiji

Klabu ya Dodoma Jiji Fc imekamilisha usajili wa kiungo Randy Bangala Litombo kutoka nchini Congo Drc ambaye anakuja kuongeza nguvu katika eneo la katikati mwa uwanja wa timu hiyo.

Viongozi wa Dodoma Jiji Fc wameshawishika kumsajili Randy baada ya kuvutiwa na kiwango chake alipokua akiichezea timu ya Insta United kwenye michuano ya Ndondo Cup ambapo pia timu ya Polisi Tanzania ilikua ikiwania saini ya mchezaji huyo.

Dodoma jiji imekua na msimu mzuri tangu ipande ligi kuu tofauti na klabu zingine ambazo zikipanda daraja zimeshindwa kudumu katika fomu zao na kusababisha kukaa msimu mmoja na kushuka daraja ama kuponea kwenye play Off.

Bangala ambaye ni ndugu na kiungo wa Yanga sc Yannick Bangala tayari ameshajiunga na kambi ya mazoezi ya klabu hiyo jijini Dodoma.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala