Connect with us

Makala

Kocha Mpya Kengold Fc Usipime

Kocha mpya wa Kengold Fc Vladislav Heric amekuja Tanzania akiwa na Jukumu la kuhakikisha wakazi wa Chunya wanaendelea kuiona timu yao katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Heric ni miongoni mwa makocha wanaolijua vyema soka la Afrika ingawa Maisha yake amezifundisha timu nyingi za Afrika Kusini ambapo alifanya vizuri kulingana na aina ya timu alizokua akizifundisha.

Akiwa Afrika kusini alijijengea Jina la bingwa wa kupandisha timu ambapo alipandisha timu mara nyingi katika ligi kuu na alizinusuru timu kwenye Janga la kushuka daraja Mara tisa.

Hata hivyo itakua kazi kwake kuendeleza historia yake ya kunusuru timu kushuka daraja ambapo timu yake ya Kengold Fc inakabiriwa na hatari ya kushuka daraja kutokana na kushikilia mkia katika msimamo wa ligi kuu nchini.

Katika michezo ya ligi kuu ya Nbc nchini timu hiyo mpaka sasa imecheza jumla ya michezo  16 ikiwa na alama 6 pekee ambapo imeshinda mchezo mmoja pekee.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala