Connect with us

Makala

Julio Alalama Kipigo cha Azam Fc

Kocha msaidizi wa klabu ya Namungo Fc Jamhuri Kihwelo amelalamika kuwakosa baadhi ya wachezaji wake wa mkopo katika mchezo dhidi ya Azam Fc ambapo klabu yake ya Namungo fc ililala kwa mabao 2-1 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ilula mkoani Lindi.

Namungo Fc wakiwa nyumbani walianza kupachika bao la mapema kupitia kwa Mohamed Issa Banka dakika ya 2 lakini mtoto wa mfalme Prince Dube alisawazisha dakika ya 22 na dakika 10 kabla ya mapumziko Ismail Aziz Kadar alifunga bao la pili na kuimaliza mechi kipindi cha kwanza.

Juhudi za Namungo kusawazisha hazikuzaa matunda mpaka dakika 90 za mchezo zinakamilika ambapo kocha Julio alilalama kuhusu suala la kuwakosa baadhi ya mastaa wake wa mkopo kutoka Azam FC.

”Mpira wa kiafrika una mambo mengi ya kishamba unakuta timu inakupa mchezaji halafu inakupa masharti tukikutana usimtumie mchezaji huyo ni nini sasa kama sio ushamba”?alilalamika kocha Julio

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala