Connect with us

Makala

Hatimae Yametia Yanga sc

Ilikua ni ahadi lakini imekua kweli baada ya klabu ya Yanga sc kufanikiwa kushinda taji la tatu la msimu huu baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho kwa kuifunga timu ngumu ya Coastal union kwa penati 4-1 baada ya sare ya 3-3 katika dakika 90 za mchezo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Coastal Union walijilipua kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo wakishambulia kwa nguvu na kukaba kwa pamoja ambapo dakika ya 22 walipata bao kupitia kwa Abdul Sopu ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza huku Feisal Salum akisawazisha dakika ya 57 na baadae dakika ya 82 Heritier Makambo akifunga bao la uongozi japo furaha ya wananchi haikudumu baada ya Abdul Sopu kufunga tena bao la kusawazisha na mchezo kumalizika 2-2 katika dakika 90 za mchezo.

Dakika ya 30 za nyongeza Abdul Sopu aliwazidi maarifa mabeki wa Yanga sc na kufunga tena bao la tatu kwa Wagosi wa kaya bao ambali nalo halo halikudumu sana kwani Dennis Nkane alifunga la kusawazisha dakika ya 113 akiunganisha shuti la Fiston Mayele na mpaka mchezo unamalizika matokeo yalikua 3-3.

Hatua ya mikwaju ya Penati iliwashuhudia Coastal Union wakikosa matuta mawili kupitia kwa Amani Kyata na Rashid Chambo huku Victor Akpam ndie pekee akifanikiwa kufunga huku Yanga sc wakifunga kupitia kwa Yannick Bangala,Heritier Makambo,Dickson Job na Khalid Aucho na kujihakikishia kutwaa taji la tatu kama ambavyo iliahidiwa na Eng.Hersi Said wakati wa kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala