Connect with us

Makala

Balaa la Azam Fc Usipime

Ni balaa ndivyo unavoweza kusema baada ya mmiliki wa klabu ya Azam Fc Yussuph Bakhresa kuamua kuinia mwenyewe kazini na kushusha vifaa vya nguvu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ambapo kwa mujibu wa bosi huyo kuwa wameamua kuchuana kunyakua taji hilo.

Balaa la kwanza la tajiri huyo asiye na mbwembwe lilianzia nchini Ivory Coast ambapo walimsainisha mkataba kiungo mshambuliaji Kipre Junior ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili huku ikisemekana kuwa amekataa ofa ya kucheza ulaya katika klabu za Ufaransa.

”Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior,Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel, tumemnunua kutokea timu ya Sol FC ya kwao, akisaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa (@yusufbakhresa) na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin (@abdulkarim.amin)”Ilisema taarifa kutoka katika mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Bila kumpumzika klabu hiyo tena ikamtambulisha Tape Edinho kutoka humohumo nchini Ivory Coast ambapo tena wakatoa taarifa inayosema kuwa “Tunayo furaha kuwataaarifu kuwa tumeinasa saini ya kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edinho, kwa mkataba wa miaka mitatu.Edinho tumemnunua kutoka timu ya ES Bafing ya kwao, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025”.

“Nyota huyo mwenye uwezo mkubwa, amesaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu hii, Yusuf Bakhresa @yusufbakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’,
Mkali huyo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) msimu huu, kutokana na ubora wake wa kuhenyesha wachezaji wa timu pinzani.Msimu uliomalizika, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano na kuchangia pasi tisa zilizozaa mabao”.Ilimalizika taarifa hiyo kuhusu usajili wa pili wa kiungo mshambuliaji.

Hawapo na hawaboi,baadae Azam Fc ikamtambulisha kocha wa makipa aliyewahi kuzifundisha klabu za ligi kuu nchini Hispania Dani Cadena,kocha huyo wa zamani wa makipa wa klabu za Ligi Kuu Hispania (La Liga) Sevilla na Real Betis atakaa Chamazi kwa misimu miwili huku pia akiwa ameshafanya kazi nchini China na Asaudi Arabia, ana uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.

Kubwa Kuliko ni pale klabu hiyo ilipomtambulisha Issa Ndala kiungo mkata umeme wa klabu ya Plateau United ambayo inayoshiriki ligi kuu nchini Nigeria kwa mkataba wa miaka miwili ambapo Kiungo huyo, mwenye umbo kubwa, sifa ya ukabaji na kupiga pasi, anakuja kuimarisha eneo la kiungo, ambapo Septemba mwaka huu atakuwa anatimiza umri wa miaka 20,Aidha mbali na kucheza Plateau, Ndalla amepita pia katika timu ya Sevan ya Armenia na Nasarawa United ya Nigeria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala