Connect with us

Makala

Morrison Is Green And Yellow

Baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu kuhusu sakata la usajili la Benard Morrison hatimaye mchezaji huyo usiku wa kuamkia leo ametambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu ya Yanga sc akirejea kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Simba sc.

Morrison amabye aliletwa nchini na Yanga sc amabpo aliwatumikia kwa miezi sita pekee kisha kuingia katika mgogoro na waajiri wake hao ambao walimfungulia kesi katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo (Cas) ambapo staa huyo alishinda kesi hiyo na kuamua mchezaji huyo ni mali halali ya Simba sc.

Baada ya kuitumikia Simba sc kwa miaka miwili mchezaji huyo alisimamishwa mwishoni mwa mkataba wake kwa matatizo ya kifamilia ambapo alipaswa kukaa nje ya timu mpaka msimu umalizike na ndipo mkataba wake utapokua umefika tamati huku uhakika wa kumuongezea ukiwa ni hafifu na ndipo alipoamua kusaini Jangwani alipoondoka kwa maneno na mgogoro wa kimkataba huku akiwaachia simanzi wananchi.

Inasemekan kuwa kurejea kwa Morrison Yanga sc ni pendekezo la kocha Nasreddine Nabi ambaye amekubali kusajiliwa kwa winga huyo huku wakimbana zaidi katika mkataba hasa masuala ya kinidhamu ambapo lengo la Nabi ni kuunda safu takatifu inayomjumuisha Aziz Ki,Morrison na Mayele.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala