Connect with us

Makala

Feisal,Mzize Wang’ara Crdb Cup

Kiungo mshmabuliaji wa klabu ya Azam Fc Feisal Salum  amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa kombe la Shirikisho huku Clement Mzize na Djigui Diarra wa klabu ya Yanga sc wakitwaa tuzo za mfungaji bora na kipa bora katika usiku wa tuzo hizo zilizotolewa na Shirikisho la soka nchini (TFF) katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam.

Feisal katika tuzo hizo akimzidi Stephane Aziz Ki wa Yanga sc na kipa Djigui Diarra ambaye wengi walitarajia kuwa anaweza kupata kutokana na kuonyesha uwezo wa juu katika michuano hiyo.

Mzize yeye alifanikiwa kupata tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kulingana mabao na Edward Songo wa Jkt Tanzania lakini alifaidika na kipengele hicho kutokana na mabao yake kuifikisha timu hiyo fainali na kunyanyua taji hilo.

Diara yeye aliwazidi Aboubakar Khomeiny na Mohamed Mustapha wa Azam Fc na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo ambayo wengi waliitarajia kutokana na mafanikio ya kipa huyo kwa siku za karibuni akiisaidia Yanga sc kutwaa taji la ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala