Connect with us

Makala

Simba Queen Watawala Tuzo TFF

Klabu ya soka ya Simba Queen imefanikiwa kutawala usiku wa Tuzo za Shirikisho la soka nchini baada ya kufanikiwa kutwaa takribani tuzo nyingi za soka la wanawake nchini katika usiku wa Tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa Super Dome Masaka Jijini Dar es salaam.

Simba queen ilikua na washiriki kutoka vipengele vya kocha bora,kipa bora,mfungaji bora na mchezaji bora ambapo ilifanikiwa kunyanya tuzo ya Mchezaji bora iliyochukuliwa na Aisha Mnuka ambaye pia alichukua tuzo ya mchezaji bora na Juma Mgunda alichukua tuzo ya kocha bora.

Kwa upande wa kipa bora wa ligi kuu ya Wanawake ilikwenda kwa Caroline Rufaa wa Simba Queen na kuifanya timu hiyo kukosa tuzo moja pekee katika ya tuzo sita ambazo iliingiza washiriki katika tukio hilo.

Msimu huu Simba Queen chini ya kocha Juma Mgunda imefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya soka ya wanawake nchini na inatarajiwa kuingia katika michuano ya kanda ili kuwania nafasi ya kuingia katika michuano ya mabingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala