Connect with us

Makala

Dtb Yabadili Jina

Klabu ya soka ya DTB iliyopanda kucheza ligi kuu nchini imebadili jina na sasa itajulikana kama Singida Big Stars huku ikihamisha makao makuu yake kutoka jijinin Dar es salaam kwenda mkoani Singida.

Timu hiyo imepanda kucheza ligi kuu msimu ujao ikiwa sambamba na Ihefu Fc baada ya kushika nafasi ya pili ambapo baada ya uamuzi wa kubadili jina hilo sasa itaitwa Singida Big Stars na itatumia uwanja wa Liti kama uwanja wake wa nyumbani.

Uamuzi wa klabu hiyo kubadili jina na kuhamia mkoani Singida umetangazwa leo na uongozi wa klabu hiyo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala