Connect with us

Makala

Simba sc Yamtimua Kocha Pablo

Klabu ya Simba sc imeachana na kocha Pablo Franco Martin baada ya kuamua kuvunja mkataba wake kama kocha mkuu wa klabu hiyo kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya jumla ya msimu huu ambapo kocha huyo hakufikia malengo aliyowekewa.

Pablo akiwa kocha mkuu wa klabu ya Simba sc aliyojiunga nayo Novemba mwaka jana akichukua nafasi ya Didier Gomez ambaye alitimuliwa sambamba na wasaidizi wake klabuni hapo alipewa malengo ya kuifikisha timu hiyo nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika huku akitakiwa kuchukua kombe la ligi kuu na shirikisho nchini.

Katika malengo hayo matatu kocha huyo hakutimiza hata moja ambapo alitolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika huku pia akitolewa katika nusu fainali ya kombe la shirikisho nchini alipofungwa na Yanga sc kwa 1-0 katika mchezo uliofanyika jijini Mwanza huku katika ligi akiwa amezidiwa alama 13 ambazo ni ngumu kuzivuka kutokana na michezo iliyosalia.

Tayari kocha huyo amepewa barua ya kuvunjiwa mkataba japo inasemekana hajasaini kutokana na baadhi ya vipengele vya kimasilahi kutokaa sawa ambapo pia sekeseke hilo limemuhusu kocha wake wa Viungo Daniel Castro.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala