Connect with us

Makala

Caf Yaipiga Nyundo Benjamin Mkapa

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limeamua kuufungia uwanja wa Benjamini Mkapa kutokana na sehemu ya kuchezea ya uwanja huo kutokua na ubora unaohitajika kwa mujibu wa viwango vya ubora wa Shirikisho hilo.

Katika barua iliyoandikwa na Caf Kwenda kwa shirikisho la soka nchini (TFF) imeonyesha kuwa uwanja huo umeharibika katika eneo lake la kuchezea hivyo limetoa muda kwa ajili ya kuufanyia marekebisho kabla ya kutuma wakaguzi ambao watakuja kuugakua kisha watatoa ripoti kama unafaa ama lah.

Hivyo kutokana na taarifa hiyo,Caf pia limeitaka TFF kuhakikisha klabu ya Simba sc inachagua uwanja mwingine wenye hadhi ya Caf kwa ajili ya mchezo wake wa hatua ya kwanza dhidi ya Al-Masry ya nchini Misri ambao hapo awali ulipangwa kufanyika uwanjani hapo.

Simba sc na Al-Masry ilikua zikutane uwanjani hapo April 9 2024 katika mchezo war obo fainali ya kombe la shirikisho lakini sasa klabu hiyo itapaswa kuchagua uwanja mwingine wenye hadhi ya Caf ambapo vinapatika ama nchini Uganda au Rwanda uwanja wa Amahoro.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala